FUGA KUKU WA MAYAI NA SIRI ZA JAMII: FAHAMU MAMBO YA KUFANYA



Kama unawazo la kufuga kuku ni wakati wako mzuri kupata ujuzi na umekuwa mtu wa bahati kutembelea ukurasa wetu wa siri za jamii naweza kusema msomaji wangu upo mahala sahihi.



kuku unaweza kufuga mtu yoyote yule cha msingi ni kuwa mbunifu na kujua ni nyakati gani na maeneo gani rafiki ya kuanzisha ufugaji, kila biashara inaitaji ubunifu ili ata iweze kuvutia wateja na uweze kujipatia kipato chako cha kila siku na katika mwaka 2016 katika maonesho ya wakulima morogoro yaliofanyika eneo la nane nane tulikutana na ufugaji kuku wa mayai na kupata maelekezo sahihi kutoka kwa wataalamu wakatuelewesha jinsi ya kuandaa mabanda na kufuga kuku wa mayai



kuku wa mayai haya ndio mabanda ambayo yametengenezwa pia hayawezi kumpa shida mfugaji kukusanya mayai, na pia kuna tabia ya baadhi ya kuku wanadonoa mayai na kuyala baada ya kutaga kwa sababu hyo mtindo wa mabanda ya aina hii itakuwa ni suluhisho kubwa kwa mfugaji na kuyalinda mayai katika kupata uharibifu.




Pia kama unavyojua familia zetu za kiswahili uwaga atunaga maeneo makubwa ya kufanyia mambo haya kwa kusema ivyo mabanda ya aina hii unaweza kuwa nalo hata katika nyumba za kupanga pia yanaweza kuimili wale wafugaji walio na kuku wachache pia ukiwa nalo ata moja sio mbaya utakuwa umepiga atua katika ufugaji wa kuku wa mayai.

 

Katika njia za ufugaji zipo njia mbali mbali ambazo ukionana na wataalamu wa mambo ya ufugaji wa kuku wa mayai utakutana na mambo mengi mazuri na itasaidia kuanza ujasiriamali wenye tija ata katika jamii yako na pia wanajamii pia ni jambo zuri kutembelea maonesho ya kilimo katika eneo lako husika unaweza kukutana na fursa ambazo zinaweza kubadilisha maisha yako.



No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.