FAO LA KUJITOA NA UFAFANUZI WAKE KIUNDANI
Posted by
Jackson Msuya on
Tuesday, 13 sept,2016
Ni fao kwa maana ya fedha zitolewazo na mfuko flani wa hifadhi za jamii kwa wateja wao walioamua kujitoa kwenye mfuko husika kwa sababu mbalimbali mfano
1) kutoridhiwa na huduma za mfuko husika hivyo kuamua kujitoa ili kuamua kujiunga na mfuko mwingine wa kijamii.
2) kuacha au kupunguzwa kazi kwa mwajiri wake wa awali hiyo huomba fao la kujitoa ili kufanya shughuli nyingine
Fao la kujitoa(WITHDRAW FUND) Hutolewa kwa mfanyakazi yeyote ambaye ni mteja wa mfuko husika na mwajiri wake amekuwa akichangia michango yake yote kwenye mfuko kwa muda wote aliokuwepo katika ajira husika.
Je? FAO HILI LINATAMBULIKA KISHERIA?
Kwa msingi fao hili halijaanzishwa na sheria yeyote tukianzia sheria ya MAMLAKA YA HIFADHI ZA KIJAMII NO.8 YA MWAKA 2008, LAKIN PIA SHERIA YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI ZA JAMII NO. 50 KAMA ULIVYOFANYIWA MAREKEBISHO MWAKA 2015 KIFUNGU NAMBA 21 kinaeleza bayana aina za mafao ambayo mfuko hilipa ambayo ni
1) Retirement pension (fao la kustaafu)
2) Invalidity pension
3) Survivors pension ( fao la wategemezi)
4) Funeral grants. (Gharama za mazishi) na nyinginezo.....
Hivyo tunaposema fao la kujitoa limefutwa lazima tujiulize limeanzishwa na sheria gani na kimsingi halipo umekuwa ni utaratibu tu usiotambulika kisheria hivyo binafsi naunga mkono HOJA ZINAZOTOLEWA NA NSSF TANZANIA
Leave a Comment